Dada wa msanii Diamond Platinumz amefunguka na kukanusha kauli yake aliyowahikusema hapo awali kuhusu kumpenda wifi yake mpya tanasha ambae ndie anakwenda kuwa kuolewa mwaka 2019 na msanii huyo.
Hapo awali mwanadada huyo alisema kuwa anampenda sna wiifi yake na wanamkaribisha katika familia yao lakini ghafla mwanadada huyo amegeuka na kusema kuwa hamjui kabisa mwanadada huyo na kwamba mwanadada huyo hajatambulishwa kwao hivyo hawezi kusema chochote.
Esma anasema kuwa hajawahi kutambulishwa zaidi ya kumjua kutoka instagram , kwa hivyo wala hajui kitu na yeye anaona ni kama msinema tu.
Alipoulizwa kuhusu ni kitu gani anaenjoy kutoka kwa wifi yake Tanasha majibu ya Esma yalikuwa “ndugu yangu sina hata ninachoenjoy kutka kwa tanasha,kwa sababu simjui na yeye hanijui wala kwaio tumekuwa tukionana tu huku instagram, lakini ukinuliza wala sijui chochote.bado hatujatambulishwa rasmi na sisi tunaona sinema kama nyinnyi mnavyoona tu.”