EU yalaani balozi wake kufurushwa DRC

EU yalaani balozi wake kufurushwa DRC
Muungano wa Ulaya umeuakosa uamuzi wa Jamhuri ya Demokrasi wa kumfukuza balozi wake kabla ya uchaguzi muhimu nchini humo siku ya Jumapili.

"Amri ya kumtaka Bart Ouvry kuondoka ndani ya saa 48 ni kinyume kabisa na sheria", msemaji wa EU alisema.

DR Congo ilisema ilichukua uamuzi huo kulipiza vikwazo vilivyowekewa mgombea wa chama tawala Emmanuel Ramazani Shadary.

Maandalizi ya uchaguzi huo yamekumbwa na ghasia.


Siku ya Alhamisi wafuasi wa upinzani walisaka kituo cha Ebola kwenye mji ulio mashariki wa nchi wa Beni kupinga uamuzi wa tume ya uchaguzi wa kuhairisha uchaguzi kwenye miji mingine miwili hadi mwezi machi.

Ghasia pia zilikuka kwenye miji miwili ngome za upinzani za Goma na Butembo iliyo yote mashariki mwa nchi.

Kichanga cha siku 6 chapona Ebola
Tume ya uchaguzi ilisema uchaguzi kwenye mji wa Beni, Butembo na mji ulio magharibi wa Yumbi utaharishwa hadi Machi kwa sababu ya ukosefu wa usalama na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola eneo la mashariki umesababisha vifo vya zaidi ya wtu 300.

Haki miliki ya pichaREUTERS
Image caption
Maafisa wa uchaguzi wamekuwa wakifanyia majaribio mashine kabla ya uchaguzi
Kipi kilisababisha kuzika mzozo wa kidiplomasia?
Vikwazo kwanza vilitangazwa dhidi ya Bw Shardary mwaka 2017 kwa ukiukaji wa haki za binadamu ikuwemo hatua kali dhidI ya upinzani.

Tarehe 10 Desemba mawaziri wa EU waliongeza vikwazo hivyo vikiwemo wa kuzuia mali na marufuku ya kusafiri kwa Bw Shardary na watu wengine 13 kwa kuhujumu uchaguzi na ukiukaji mwingine wa haki za binadamu.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad