Haji Manara ageuka kuwa mlinzi wa Simba

Haji Manara ageuka kuwa mlinzi wa Simba
Mkuu wa kitengo cha habari wa klabu ya Simba, Haji Manara alikuwa ni miongoni mwa viongozi waliosafiri na timu kwenda eSwatini lakini hakutazama dakika 45 za kwanza kutokana na kuwa mlinzi wa chumba cha kubadilishia nguo.


Manara amesema muda wote wa kipindi cha kwanza alijipa jukumu la kuwa mlinzi ili kuepusha chumba chao kuhujumiwa kutokana na historia ya matukio ya aina hiyo katika soka la Afrika.

''Kiukweli 'first half' sikuona kabisa mechi, nilijipa jukumu la kulinda chumba chetu cha kubadilishia nguo wachezaji wetu, soka la Afrika lina vitimbi vingi sana ndani na nje ya uwanja, ila sisi tulijipanga.'', alisema Manara.

Moja ya tukio ambalo huenda lilimfanya Manara akae na kulinda chumba cha kubadilishia nguo ni lile lililowatokea Azam FC mwaka 2017 walipokutana na Mbabane ambapo vyumba vilipuliziwa dawa iliyowamaliza nguvu wachezaji katika kipindi cha pili na kupelekea kupoteza kwa 3-0.

Katika mchezo wa jana, Simba ilishinda kwa mabao 4-0 hivyo kufikisha jumla ya mabao 8-1 na kusonga mbele katika hatua ya kwanza na klabu bingwa Afrika ambapo sasa itasubiri droo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad