Haji Manara Amwagia Sifa DC Jokate "Ni Mrembo wangu Bora Kwa Miaka Saba Mfululizo"

Haji Manara Amwagia Sifa DC Jokate "Ni Mrembo wangu Bora Kwa Miaka Saba Mfululizo"
Mwaka ukiwa unaelekea ukingoni  leo Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano ndani ya klabu ya Simba, Haji Manara ameweka hadharani orodha ya wanasanaa mbalimbali walioukonga moyo wake.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Manara amesema kwa mwaka 2018, Mwanamuziki  Mwanafalsa pamoja na Maua Sama wameisuuza nafsi yake vilivyo kupitia wimbo  wa 'Silewi' ambao kwake ameuita ni wimbo bora wa Hip hop.

Manara ameeleza kuwa msanii wake bora wa kike ni mwanadada Nandy 'The African Princess' huku akidai kwamba wimbo wake bora wa Bongofleva anaogopa kufungiwa Basata "nikiitaja tu nnao"

Manara ameongeza kwamba mrembo wake bora kwa mwaka wa saba mfululizo ni Jokate Mwegelo ambaye kwa sasa ni Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe huku Flaviana Matata akiwa mwanamitindo bora.

Kwa upande wa filamu Manara amemtaja Jacob Stephen 'JB' kama muigizaji bora wa filamu wakiume huku Riyama Ally akichukua nafasi kwa waigizaji wakike.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad