Ofisa habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa wapinzani wao Yanga inabidi watulie kwanza kuhusu viporo vyao walivyonavyo Ligi Kuu, watarejea kumaliza baada ya kucheza michezo ya kimataifa.
Manara ameyasema hayo kutokana na Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera kuhoji sababu ya viporo vya wapinzani wao licha ya kumaliza kucheza hatua ya awali na kurejea nchini bila kucheza tofauti na ilivyokuwa kwao wakati wakishiriki michuano ya kimataifa.
"Kwa sasa wapinzani wetu inabidi watulie kwanza tuna kazi kubwa ya kuweza kuiwakilisha nchi kimataifa, hili ni agizo tulilopewa na mheshimwa Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli, serikali inatambua kazi yetu watuache kwanza tufanye kazi tukirudi tutamalizia kila kitu," alisema.
Simba wamecheza jumla ya michezo 12 kwenye ligi kuu huku Yanga wakiwa wamecheza jumla ya michezo 15 ya Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu.
Haji Manara Awatolea Uvivu Yanga Kisa Vipolo vya Simba
0
December 11, 2018
Tags