Hapi aweka wazi sababu ya kuchelewesha kugawa vitambulisho kwa wamachinga


Mkuu wa Mkoa wa Iringa Ally Hapi ameweka wazi sababu zilizopelekea kuchelewe kwa mchakato wa ugawaji wa vitambulisho kwa wafanyabiashara wadogo mkoani humo.

 Hapi amesema hayo wakati akikabidhi vitambulisho vya wafanyabiashara wadogo kwa Wakuu wa Wilaya zote mkoani humo ili kuwagawia wajasiliamali waliokidhi vigezo.

Aidha ameongeza kuwa zoezi hilo lina sifa maalum ambapo kama mkoa walikuwa wanasubiri muongozo rasmi wa sifa na mashrtiya ugawaji ''Sio kila mtu anaweza kupata kitambulisho hicho ambapo sifa ni lazima awe na mauzo ghafi yasiyozidi milioni nne kwa mwaka"

Kwa upande wake makamu mwenyekiti wa wamachinga mkoni humo amewataka wajasiliamali kujitokeza kuchukua vitambulisho hivyo na kuachana na mambo yanayozungumzwa vijiweni kuwa havina umuhimu katika biashara zao
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad