"Sasa hivi Wasanii Wavaa Uchi Hawapo Bongo Movie" Natasha


Muigizaji mkongwe wa Bongo movie Mwanamama Natasha ambaye pia ni mama mzazi wa Msanii Ivyonne Cherry ‘Monalisa’ amefunguka na kudai Hivi sasa Bongo movie hakuna wasanii wanaovaa uchi badala yake wamehamia kwenye tasnia ya Bongo fleva.

Kwenye mahojiano aliyofanya na kipindi cha Enews cha EATV, Natasha ameshukuru BASATA kwa kusimamia hilo na kuhakikisha inadhibiti wavaa utupu wote:

Baada ya Baraza la sanaa kusimamia vizuri na kuchukulia hatua wasanii waliokuwa wakitumia kiki mpaka kuvua nguo kwa sasa wasanii hao wametoweka na wamehamia kwenye muziki kitu ambacho kwa sisi Bongo Movie tunajivunia”.

Lakini pia nguli huyo amefunguka kwamba kwa upande wake anaona kwa mwaka 2018 kazi za filamu Tanzania zimelipa sana tofauti na miaka ya nyuma.

Kwa kweli mimi nimekuwepo tangu miaka ya makundi ya Kaole mpaka sasa na kwa mwaka huu naweza nikasema huu mwaka umekuwa na neema na baraka kwa waigizaji kwani umeleta mafanikio mengi ikiwemo ongezeko la wanunuzi wa mtandaoni kitu ambacho kimeinua soko la filamu”.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad