Iggy Azalea aendelea kutumbuiza baada ya dancer wake kuanguka jukwaani


Fahamu kuwa mmoja wa dancers wa Rapper Iggy Azalea alianguka ghafla jukwaani usiku wa December 27,2018 nchini Brazil na kuelezwa kuwa ni kutokana na hali ya joto pamoja na mwanga.

Gumzo lilizuka baada ya Iggy kuonekana akiendelea kutumbuiza kwenye jukwaa hilo huku akiimba wimbo wa ‘Black Widow’ wakati dancer wake akiwa chini hajitambui ila baadae alionekana akiomba muziki uzimwe ili dancer wake apatiwe huduma ya kwanza.


Baada ya show Iggy aliandika ujumbe kupitia Insta story yake na kuwataka mashabiki wafahamu kuwa dancer huyo alikua akiendelea vizuri na kutoa sababu ya kuzimia huku akitaja kuwa ni kutokana na hali ya joto pamoja na taa.

Iggy Azalea aliongeza na kusema kuwa alihisi kuwa dancer wake alianguka tu kutokana na kuteguka mguu lakini kuimba kunaendelea mpaka wimbo utakapoisha ndio daktari anaitwa na ndicho alichofanya.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad