Irene Uwoya ahamishia majeshi kwa AliKiba


Mwanadada mwenye mvuto wa aina yake kwenye tasnia ya sinema za kibongo, Irene Uwoya amesema kuwa anamkubali mwanamuziki Alikiba, huku akitaja wimbo wa 'hadithi' kuwa ndio wimbo wake pendwa wa muda wote.

Uwoya amefunguka hayo baada ya kuonekana kwenye tamasha la msanii huyo la kufunga mwaka, ambapo amesema kuwa hajawahi onekana akiwa karibu na Kiba lakini ni mtu anayeikubali kazi yake.

"Alikiba ni mtu nnayemkubali, ninapenda nyimbo zake na ndio maana nimekuja hapa leo", amesema Uwoya.

Mwanadada huyo pia amezungumzia kuhusiana na suala la kuzindua 'Pub' yake aliyotarajiwa kuzindua usiku wa tarehe 23 lakini amesema kuwa hakufanya hivyo kwakuwa kuna vitu havikukamilika kwa wakati.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad