Jerry Muro awatupia dongo Simba

Jerry Muro awatupia dongo Simba
Jerry Muro aliyewahi kuwa Ofisa Habari wa Yanga ameibuka baada ya kuwa kimya kutokana na majukumu ya Ukuu wa Wilaya ya Arumeru ambayo alipewa hivi karibuni kwa kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli.

Muro ameeleza hayo ikiwa ni baada ya ushindi wa mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya African Lyon wa bao 1-0 uliopigwa jana kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.

"Unajua sisi bado ni wa kimataifa halisi, mpaka sasa bado hatujapoteza mchezo hata mmoja, tunaendelea kuonesha ukimataifa tofauti na wale wenzetu wa matopeni, ikumbukwe hadi leo hatujapoteza hata mchezo mmoja" alisema Muro.

Aidha, Muro amemtumia salaam Manara alimweleza wajiandae kupokea kipigo kwenye mzunguko wa raundi ya pili akiamini moto walionao Yanga hivi sasa si wa kuotea karibu.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad