Jeshi la Polisi Latangaza Vita kwa Wezi was Mafuta Ujenzi wa Reli

Jeshi la Polisi Latangaza Vita kwa Wezi was Mafuta Ujenzi wa Reli
Jeshi la Polisi nchini, limetangaza kuanza kwa Operesheni kali ya kuwasaka watu wote wanaojihusisha na wizi wa mafuta katika mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) unaoendelea kutoka Dar es Salaam kwenda Morogoro.


Hayo yamesemwa na Mkuu wa Operesheni Maalum za Polisi, Naibu Kamishna wa Polisi DCP Liberatus Sabas, wakati akizungumza kwa nyakati tofauti na wafanyakazi wanaofanya kazi katika mradi wa reli hiyo katika kambi ya ujenzi ya Soga mkoani Pwani na Ngerengere wakati wa ziara yake katika mradi huo kufuatia kuwepo kwa vitendo vya wizi wa mafuta.

Sabas amesema Operesheni hiyo haitamwacha salama yeyote atakayekutwa akishiriki na kufanikisha vitendo vya wizi katika mradi na kuwataka wafanyakazi hao kuwa wa kwanza kutoa taarifa pindi waonapo viashiria vya wizi katika maeneo yao ili mradi uwe salama.

“Polisi tutatumia kila aina ya nguvu zetu kuhakikisha kuwa mradi huu unakuwa salama na tukikamata mwizi wa mafuta katika mradi huu hatasahau maisha yake yote kwa kuwa kuhujumu mradi huu muhimu kwa taifa ni kosa kubwa hasa ukizingatia gharama kubwa ambazo Serikali inatumia kufanikisha jambo hili” Alisema Sabas.

Katika hatua nyingine DCP Sabas amewaelekeza Makamanda wa Polisi wa mikoa ya Pwani na Morogoro kuweka mikakati kabambe kwa kushirikiana na Kikosi cha Polisi Reli ili kufanya doria za mara kwa mara katika vijiji vinavyozunguka mradi huo kwa kuwa ndipo kulikobainika kuuzwa mafuta ya wizi wa mradi huo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad