Jeshi la Polisi Mwanza Lakamata Majambazi Watano Wakiwa na Noti Bandia Milioni 2

Jeshi la Polisi Mwanza Lakamata Majambazi Watano Wakiwa na Noti Bandia Milioni 2
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza kwa kushirikiana na kikosi kazi kabambe cha kanda ya ziwa chenye uwelediwa hali ya juu na chenye uaminifu uliotukuka tukishirikiana na Maofisa wa Tanapa –Serengeti. Tumefanikiwa kuwakamata jumla ya majambazi watano sugu wakiwa na noti bandia zenye thamani ya kiasi cha Milioni mbili laki nane na elfu thelasini (TSH 2,830,000/=) na vifaa mbalimbali vya kutengenezea fedha hizo huko mtaa wa Kiloleli B, kata ya Nyasaka Wilayani Ilemela, kitendo ambacho ni kosa la jinai.

Katika operesheni hiyo maalumu iliyochukua takbrani masaa 48 kuanzia tarehe 03/12/2018 majira ya 04/04/2018 imefanyika baada ya kupatikana kwa  taarifa za kiintelejensia kwamba katika mtaa wa Kiloleli B wapo watu wanaotengeneza noti bandia.

Baada ya kupatikana kwa taarifa hizo kikosi hicho maalumu cha askari wa mikoa ya kanda ya ziwa toka Mkoa wa Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Mara na Tanapa –Serengeti kilifanya msako mkali katika mtaa huo na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa tajwa hapo juu wakiwa na kiasi hicho cha noti bandia.

Watuhumiwa wawili  wamekamatwa maeneo ya Mugumu Serengeti ambao ni;
Swedi Amani Mrete @ Kongo, miaka 40, mfanyabiashara, mkazi wa buhongwa Mwanza
 Cosmas Busiga Bereka, miaka 40, fundi chuma, Mkazi wa Mandu Mwanza.
Aidha watuhumiwa wengine wawili wamekamatwa mtaa wa Kiloleli B kwenye nyumba ambayo ndipo wanapotengenezea fedha hizo bandia ambao ni;
Baraka Dominiko @ Mwanga, miaka 26, mfanya biashara, mkazi wa kiloleli B.
 Khadija Musa Elias, miaka 20, mkulima, Mkazi wa Kiloleli B.
Vilevile mtuhumiwa aliyetoroka amekamatwa huko mto Malagarasi Kasulu Kigoma, mtuhumiwa huyo ni;
 Batisti Msafiri Katumbi, miaka 40, mfanya biashara, mkazi wa Igoma Mwanza
Sambamba na hilo watuhumiwa hao wamekamatwa wakiwa na noti hizo bandia zikiwa katika makundi yafuatayo;
  Noti za elfu kumi zimekamatwa zenye thamani ya  kiasi cha laki mbili na elfu thelasini (TSH 2,230,000)
 noti za elfu tano zimekamatwa zenye thamani ya laki nne na elfu sabini (TSH 470,000/=)
 Noti za elfu mbili zimekamatwa zenye thamani ya  elfu sitini ( TSH 60,000/=).
  Noti za dola mia kumi na nne.
  Jumla kuu TSH 2,830,000/=
Aidha watuhumiwa hao wamekamatwa wakiwa na vifaa vifuatavyo vya kutengenezea noti hizo bandia.
    Mashine moja ya printer aina ya HP.
    Paper cutter moja
    Pasi tatu za umeme
    Cartilage nane
    Ink refuels chupa nane.
    Sirinji /Sindano 4 na
    Rim paper
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza, tunaendelea na mahojiano na watuhumiwa wote watano pindi uchunguzi ukikamilika  watafikishwa mahakamani. Pia msako mkali wa kuwatafuta watuhumiwa wengine ambao walifanikiwa kutoroka bado unaendelea katika maeneo yote ya Jiji na Mkoa wa Mwanza na maeneo ya Mikoa Jirani.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza tunatoa onyo kwa baadhi ya wananchi wanaojihusisha na utengenezaji wa noti bandia kuwa waache tabia hiyo mara moja kwani ni kosa la jinai na endapo mtu atabainika hatua stahiki za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.

 Sambamba na hilo tunaendelea kutoa wito kwa wananchi waendelee kutoa ushirikiano kwa kutupa taarifa mapema za uhalifu na wahalifu ili waweze kukamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria. Wananchi wawe makini, fedha hizo zingeingia mtaani zingeleta kilio kikubwa sana tena sana.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad