Akizungumza leo Desemba 24 katika mkutano na waandishi wa habari, uliolenga kuelezea hatua ambayo mchakato wa tuzo hizo umefika, Jakate ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, amesema watu hawapaswi kuangalia umaarufu kama kweli wanataka kukuza Sanaa hiyo na badala yake waangalie uwezo na kipaji cha mtu.
Amesema kwa kufanya hivyo kutasaidia pia kuja na vipaji vipya badala tasnia hiyo kutawaliwa na watu walewale kila siku na kupongeza hatua ya waandaaji ya kwenda hadi mikoani kusaka washiriki.
“Pamoja na kwamba waandaji wameamua kutoa nafasi kwa watengeza filamu kutoa majina ya wale wanaowaona ni bora katika kipengele cha muigizaji bora wa kike na wa kiume, lakini hii katika upigaji kura haiwazuii kuchagua mnayemuona anafaa, na nina imani hata hao waandaaji hawatatuletea mtu ambaye wanajua hastahili." Amesema