Mchezaji wa klabu ya Manchester United na taifa la Uhispania Juan Mata amefunguka na kutoa ya moyoni.
Mchezaji huyo ambaye ilidaiwa kuna na tofauti na kocha wa zamani wa klabu hiyo Mreno Jose Morinho ambaye alifanya nae kazi Chelsea na baadaye koch huyo kumuuza Mata United lakini baada ya takribani misimu miwili Mourinho alifukuzwa Chelsea na kujiunga na United ndipo alipokutana na Mata tena.
Baada ya kujiunga na United watu wengi walidhani Mata hatapata nafasi ya kucheza tena Man United kama ilivyokuwa Chelsea na ndivyo ilivyokuwa kwani mchezaji huyo hakuwepo katika mipango ya kocha huyo kwa katika michezo mingi Mata alikuwa anaanzia benchi.
Baada ya kuja sasa Mnorway Ole Gunnar Mata amefunguka na kusema kuwa “Kwa sasa United ni wakati wa matumaini”
Mata aliandika kwenye blog yake ya kila wiki kuwa “Mkongwe Ol Gunnar ndio Boss wetu kwa sasa, hatuweza kuanza kuwa na wasi wasi kwa timu kama ndio imeanza na nguvu mpya sasa”
“Ilikuwa ni ushawishi wake wa kushinda dhidi ya Cardiff na itatuongezea maadili mema hadi mwishoni mwa msimu 2018 na mwaka unaokaribia haraka.Ni wakati wa kuwa na matarajio, kuangalia mbele na kuendelea kufanya kazi kwa bidii ili kupanda meza.
“Kweli tumehamasika sana kufanya hivyo wakati huo tukipata burudani na mmashabiki wetu, ambao wanastahili sana.”
“Kwa Kuanza, tunacheza Siku ya Boxing day dhidi ya Huddersfield, Ni tarehe ambayo inanikumbusha siku yangu ya kwanza katika Ligi Kuu , Miaka saba iliyopita, tangu wakati huo ilibadilishwa kuwa moja ya siku bora zaidi ya mwaka katika maisha yangu.”
“Siku nne baadaye, tutakaribishwa na Bournemouth, timu ambayo ina msimu wa ajabu sana, Katika mchezo wetu wa kwanza wa ligi dhidi yao, tuliweza kushinda shukrani kwa goli la dakika za mwisho lilifungwa na Marcus, na Jumapili nina hakika kwamba watakuwa wanangalia zaidi kulipiza kisasi. “