Kama kuna kazi mpya imefanywa na Wema Sepetu baada ya kufungiwa iripotiwe - Joyce Fisoo


Katibu Bodi ya Filamu Tanzania, Bi. Joyce Fissoo ,  Bi. Joyce Fisso amesema kama kuna kazi mpya ya Wema Sepetu inayotangazwa baada ya kufungiwa kujihusisha na kazi za filamu iripotiwe. 

Fisoo ameiambia E- News  msanii huyo wamemfungia na bado wanaendelea kumfungia na wakitaka kumfungulia watafanya Press na waandishi wa habari kama walivyofanya awali. 

"Wema tumemfungia na bado tunaendelea kumfungia, tutamfungulia kwa kutoa press kama tulivyofanya, kama nilivyosema tulisema tunafuatilia mwenendo wake na kweli tunafuatilia na kuna task ambapo tumempa tunazipima tukijiridhisha kuwa amerejea kwenye nidhamu na amejitambua tutakaa na kuona cha kufanya," amesema Bi Joyce. 

"Kama kuna kazi mpya mmeiona baada ya kufungiwa umeiona naomba iwasilishwe na utaona kitakachofuatwa."

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad