Katibu Mkuu CCM Dk Bashiru Ally Akana Kumjibu Bernard Membe Mitandaoni

Katibu Mkuu wa CCM,  Dk Bashiru Ally amelikana andiko  linalosambaa mtandaoni likionyesha kuwa amemjibu aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe.

Dk Bashiru amesema andiko hilo si lake na hayupo katika mfumo wowote unaomuwezesha kuwasiliana kupitia mitandao ya kijamii zaidi ya kupiga simu na kutuma ujumbe mfupi wa maneno.

Sehemu ya andiko hilo linalosambaa kwenye mitandao ya kijamii linasema, “Zipo taarifa kwamba yupo kiongozi mmoja aliyewahi kuwa mwandamizi wa Taifa hili eti kanikosoa kuhusu utaratibu niliotumia kumwita ndugu Membe, mimi niombe hawa wastaafu watulie ili tukiweke chama sawa.”

“Na nirudie tu kusema ndugu Membe kama atakuwa hajafika ofisini kabla ya tarehe 17 na 18, 2018 nitakiomba kikao cha kamati kuu ya NEC kimwazimie.”

Dk Bashiru amesema waliofanya hivyo ni wale waliozoea kuendesha nchi kiholela na bado watazua mengi.

 “Watu wanaonijua wanafahamu jinsi ninavyotumia simu, sipo huko na  sina Instagram, Twitter, WhatsApp, Facebook wala mfumo wa barua pepe kwenye simu yangu, ni wazushi hao puuzeni hizo habari, ”amesisitiza.

==>> Hili ndo andiko linalosambaa mitandaoni

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad