Kauli ya kibabe ya Simba kuhusu mashindano ya Kimataifa


Kufa na kupona ni kauli ya kibabe ambayo ilifanikiwa kuivusha Simba kwenye hatua ya kwanza mpaka makundi kutokana na hamasa iliyofanywa na Ofisa habari wa Simba Haji Manara kwa mashabiki na kufanikiwa kujitokeza kwa wingi uwanjani kuwapa hamasa wachezaji. 

Manara aliibua kauli hiyo baada ya Simba kupoteza mchezo wa kwanza wakiwa ugenini mbele ya Nkana FC ambayo mtanzania Hassan Kessy anaichezea kwa kuchapwa bao 2-1 na katika mchezo wa marudio walifanikiwa kupata ushindi wa mabao 3-1. 

Manara sasa ameamua kuja na kauli nyingine ya kishujaa kwa ajili ya kuweza kuvuka hatua ya makundi na kufika robo fainali ambayo ameipa jina la inawezekana. 

"Ratiba kwa upande wetu ni nzuri, tunaanzia nyumbani na kumaliza makundi nyumbani pia, mashindano haya ni makubwa kwa ngazi ya vilabu na tuanze uwekezaji makhususi kwa ajili ya Championi Ligi, tunaweza hii ndio kampeni na kauli yetu," alisema Manara. 

Simba wamepangwa kundi D katika Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu ikiwa ni timu pekee kutoka ukanda wa Afrika Mashariki kwenye michuano hiyo mikubwa inayotarajiwa kuanza Januari 11.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad