Kimenuka Kakolanya Amponza Kigogo Yanga

Kimenuka Kakolanya Amponza Kigogo Yanga
MAMBO ni moto ndani ya Yanga. Hivyo ndivyo u n a v y o w e z a kusema baada ya kigogo mmoja wa klabu hiyo kukumbana na balaa kutoka kwa kocha mkuu wa timu hiyo, Mkongomani, Mwinyi Zahera.


Unajua ilikuwaje? Baada ya kipa wa timu hiyo, Ramadhani Kabwili kuumia katika mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya African Lyon ulichezwa Alhamisi iliyopita, huko jijini Arusha kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, kigogo huyo alimpigia simu Zahera ambaye yupo nchini Ufaransa na kumfahamisha juu ya tukio hilo kisha  kumuomba amsamehe Beno Kakolanya ili aweze kurudi kundini na kuendelea kuitumikia timu hiyo.



Ikumbukwe kuwa hivi karibuni Zahera alisema kuwa hataki kufanya kazi na Kakolanya katika kikosi cha Yanga kutokana na kitendo chake cha kugoma kuitumikia timu hiyo mpaka alipwe madai yake ambayo anaidai klabu hiyo jambo ambalo lilimkera vilivyo kocha huyo na kumuona kama msaliti kwa sababu si yeye pekee aliyekuwa anadai, hata wachezaji wenzake wengi klabuni wanadai lakini hawakugoma na wanaendelea kuitumikia timu hiyo kama kawaida.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad