Hii ni kutokana na kina cha bahari ya Hindi katika eneo la Mnazi Bay, Msimbati mkoani Mtwara kuendelea kumomonyoka siku hadi siku kuelekea nchi kavu
Naibu Mkurugenzi Kampuni ya Maurel & Prom Tanzania inayohusika na kuchimba gesi, Elias Kilembe amemueleza hayo Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani jana alipotembelea visima hivyo
Kilembe amesema siku hadi siku bahari inasogea nchi kavu kuelekea kilipo moja ya kisima cha gesi na mitambo hali inayowapa wasiwasi
Dkt. Kalemani amesema hali halisi inaonekana na hakuna haja ya utafiti, bali kinachotakiwa kufanyika ni kujengwa kwa ukuta haraka ambao utatenganisha kisima kilipo na bahari
Asisitiza “Kuanzia sasa anzeni kufanya utaratibu wa kujenga ukuta kwa sababu mtafika mahali mtakosa hata pa kuweka ukuta maji yakishafika, ni vizuri kuanza sasa"