Klopp Azitaja Timu Ambazo Ziko Kwenye Mbio za Ubingwa, Aitosa United

Klopp azitaja timu ambazo ziko kwenye mbio za ubingwa, aitosa United
Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp amesema “hakuna mtu anayetakiwa kujiona ameshasalimika” katika mbio za ubingwa wa Premia huku akisisitiza kuwa klabu za Chelsea na Arsenal bado zingali katika mbio za ubingwa.


Kikosi cha Klopp kitafikia nusu ya msimu kesho Disemba 26 huku kikiwa kinaongoza msimamo wa ligi baada ya kutanua pengo la uongozi kwa alama nne dhidi ya Manchester City.

Chelsea na Arsenal, wapo katika nafasi ya nne na tano mtawalia katika msimamo wa ligi na wameanchwa nyuma kwa alama 11 na Liverpool maarufu kama Majogoo wa Jiji. Klabu zote zimebakiza michezo 20 ya kuminyana.

“Hakuna mtu anayetakiwa kujiona ameachwa kwenye mbio za ubingwa,” amesema Klopp.


Katika misimu nane kati ya 10 iliyopita, klabu iliyokuwa ikiongoza ligi wakati wa Krismasi walishinda ubingwa mwisho wa msimu.

Mara mbili ambazo haikuwa hivyo mwaka 2008-09 na 2013-14 – Liverpool ndiyo walikuwa wakiongoza ligi kipindi kama hiki na kuanguka na kumaliza katika nafasi ya pili mwishoni mwa msimu.

Liverpool, ndiyo timu pekee mpaka sasa ambayo haijapoteza mchezo katika ligi ya Premia na kesho watawaalika Newcastle United katika dimba la Anfield.

Mkufunzi huyo raia wa Ujerumani ametoa kauli hizo baada ya kocha wa Tottenham Mauricio Pochettino kusema kuwa Liverpool na Manchester City ndio wenye nafasi kubwa zaidi ya kushinda taji la msimu huu.

Pochettino aliyasema maneno hayo baada ya timu yake kuibuka na ushindi wa goli 6-2 dhidi ya Everton, ushindi ambao umepunguza pengo kati yao na City kufikia alama mbili na kusalia nyuma kwa alama sita dhidi ya Liverpool.


“Nimeuona mchezo dhidi ya Everton – ambao walionesha kiwango cha zaidi ya kawaida – huku wao [Spurs] wakigongelea kila palipohitajika, na ilikuwa ni vizuri mno kila ambacho Tottenham walifanya,” amesema Klopp.

“Hali kama hiyo itatokea kwa Arsenal na Chelsea.

“Kwangu, wao [Tottenham] hawakuwahi kuwa nje, hivyo kwanini watu washangae kwamba wapo ndani sasa?


“Timu nyingi zimo kwenye hicho mukiitacho mbio za ubingwa, na hivyo ndivyo itakiwavyo kuwa.”
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad