La Liga walishtaki shirikisho la soka kisa Barca

La Liga walishtaki shirikisho la soka kisa Barca
Ligi kuu soka nchini Marekani chini ya Rais wake Javier Tebas, wamefikia uamuzi wa kulishtaki shirikisho la soka nchini Hispania (RFEF) wakishinikiza libadili uamzi wa kupeleka nchini Marekani mchezo wa La Liga kati ya Barcelona na Girona.


La Liga wamefungua kesi katika mahakama ya kiraia jijini Madrid wakiomba kwa msaada wa mahakama RFEF isaini kufuta mpango huo na mechi hiyo ambayo inatakiwa kuchezwa mjini Miami ibaki nchini Hispania kama kawaida.

"La Liga tumeamua kufungua kesi mahakamani kwasababu moja ya mamlaka zenye uamuzi wa mwisho kuhusu mchezo huo kupelekwa Miami ni RFEF na wamekuwa kimya wakati mchezo unatakiwa kuchezwa Disemba hii," amesema msemaji wa ligi hiyo.

Moja ya sababu ya La Liga kwenda mahakamani wakati huu ni kutokana na RFEF kukubali kuipokea fainali ya mkondo wa pili wa Copa Libertadores itakayopigwa kwenye uwanja wa Real Madrid Desemba 9 hivyo wanafikiri inaweza ikawa ni makubaliano ya kubadilishana mechi.

Umoja wa wachezaji nchini Hispania (AFE) nao umeripotiwa kupinga mechi hiyo kwenda kuchezewa nchini Marekani ambapo Rais wake, David Aganzo amesema hatarajii kuona mchezo wowote wa ligi hiyo ukitoka nje ya Hispania.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad