Lowassa ajibu madai ya kupongezwa na Kusifiwa mara Kwa Mara na CCM

 Lowassa ajibu madai ya kupongezwa na Kusifiwa mara Kwa Mara na CCM
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa zamani wa Jimbo la Monduli, Edward Lowassa amejibu madai ya kuonekana kiongozi pekee wa upinzani ambaye amekuwa akisifiwa mara kwa mara na viongozi wa Chama cha Mapinduzi CCM na serikali hali ambayo imeonekana kuzua sintofahamu kwa wadau wa siasa nchini.

Akijibu madai hayo Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Edward Lowassa amesema “kuhusu madai ya mimi kusifiwa na viongozi wa serikali na CCM, naacha wananchi wahukumu na mimi naamini nina nia njema na nia njema itaendelea kuwepo, anayetaka kufikiria hivyo ni hiyari yake, huwezi kumnyima binadamu kufikiria, ila ninachosema mimi sina mpango wa kuondoka CHADEMA.”

Lowassa ambaye alishawahi kuwa mgombea Urais kwenye Uchaguzi Mkuu 2015, amekuwa ni kiongozi wa upinzani pekee ambaye amekuwa akionekana kwenye baadhi ya mikutano ya serikali ambayo Rais Magufuli amekuwa akishiriki, na mara kwa mara Rais amekuwa akiompongeza kiongozi huyo ambaye alikuwa mpinzani wake kwenye kinyang'anyiro cha urais.

"Maendeleo hayana chama, ndiyo maana Mzee Lowassa yupo hapa, nikushukuru kwa utulivu wako nilipokutupa chini baada ya uchaguzi ulikaa kimya, maana tuligombea mimi na wewe lakini wengine wanapiga kelele tu, kwakweli nikupongeze kwa uzalendo," alisema Rais Magufuli kwenye uzinduzi wa maktaba (UDSM) novemba 27, 2018.

Mbali na Rais Magufuli Lowassa pia alishawahi kupongezwa na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Dkt Bashiru Ally akimtaka Mbunge wa zamani wa Mtama Bernard Membe kuiga mfano wa kiongozi huyo.

Aidha Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda kwenye uzinduzi wa Maktaba alishawahi kunukuliwa kumsifia kiongozi huyo kuwa ni mtu ambaye anashiriki shughuli za maendeleo za serikali bila kujali itikadi za vyama husika

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad