Madai hayo yametolewa na Chama cha Wananchi(CUF) upande unaomuunga mkono Mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba
Wakati madai hayo yakiibuliwa, Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho upande wa Maalim Seif Sharif Hamad, Ahmed Mazrui ameeleza hana uelewa na taarifa hizo na hayupo tayari kuzizungumzia
Katibu Kamati ya Ulinzi na Usalama CUF, Khalifa Suleiman Khalifa amedai vyama 6 vya upinzani vilivyokutaka Zanzibar wiki iliyopita, moja ya ajenda yao ilikuwa namna gani Maalim Seif atakubaliana na ACT-Wazalendo
Mgogoro wa uongozi ndani ya CUF ulianza baada ya Prof. Lipumba kurejea katika uongozi mwaka 2016, ikiwa ni takribani mwaka mmoja tangu alipojiuzulu na ofisi ya Msajili kutangaza kumtambua kama Mwenyekiti