Makonda Aamua Kumsaidia Chid Benz

Makonda Aamua  Kumsaidia Chid Benz
Baada ya ukimya mrefu kwenye game ya Bongofleva, Rapa Chid Benz 'Chuma' ameeleza kwamba Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda, ameamua kumsapoti katika kazi zake kwa mwaka 2019.


Akizungumza kupitia kipindi cha Friday Night Live kinachorushwa kila Ijumaa kupitia EATV, Chid amesema yapo mambo makubwa waliyozungumza na Mkuu wa Mkoa hivi karibuni moja wapo ni kumuhimiza aache kuona aibu na badala yake aombe msaada kwa watu wake wa karibu.

"Mh Makonda mi namuita Paul ameamua kunisaidia mdogo wake, kaniambia Chidi hakuna kuona aibu ongea na watu wako, sema waambie watuchangie mimi nguvu yangu itakuwa ndogo bado inahitajika nguvu ya watu wengine" Chid Benz.

Kuhusu mipango mingine waliyoizungumza na Mkuu huyo wa Mkoa, Chid amesema kwa sasa hatoizungumzia sana bali anamuacha kiongozi huyo afanye kwanza kwa kuwa yeye ndiye ameamua kuiweka mipango hiyo.

Pamoja na hayo Chid amewaomba watanzania hasa wasanii waungane katika kuiwezesha mipango yake iweze kufanikiwa 2019 na siyo kumsema kwa mabaya kwamba amekuwa mkabaji wakati pesa zenyewe hawana.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad