Makonda Ampa Ujumbe wa Krismasi Mtoto wake Keagan

Makonda Ampa Ujumbe wa Krismasi Mtoto wake Keagan
Ikiwa leo Wakristo nchini wameungana na Wakristo kote duniani kuadhimisha sikukuu ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo, mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda ameifanya siku ya leo kuwa maalum kwa ajili ya mwanae Keagan.


Makonda amemtakia heri mtoto wake huyo wa kwanza huku akiweka ujumbe maalumu kuwa hii Krismasi yake ya kwanza ni muhimu sana kutokana na kuwa yeye ni uzao wa kwanza ambao umeagiziwa upendo kutoka kwa Mungu kama ilivyokuwa kwa Yesu Kristo mwana wa pekee.

''Merry Christmas My lovely Son hii ni Christmas yako ya kwanza na ki Imani imebeba maudhui mapana kwa maana wale aliowajua tangu Asili , aliwachagua tangu asili wafananishwe na mfano wa Mwana wake , ili yeye awe mzaliwa wa kwanza miongoni mwa Ndugu wengi'', ameandika Makonda.


Baada ya kutafuta mtoto kwa muda mrefu, Makonda na mkewe walifanikiwa kupata mtoto wa kiume na waliweka wazi juu ya hilo Julai 17, 2018.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad