Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) yatoa tahadhari ya mafuriko kwa baadhi ya mikoa


 Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa tahadhari kwa wakazi wa baadhi ya mikoa nchini humo kutokana na vipindi vya mvua kubwa zinazotarajiwa kunyesha katika siku tano zijazo.

Hayo yameelezwa leo Jumapili Desemba 16, 2018 kati  taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na mamlaka hiyo.

TMA imewataka wakazi wa maeneo ya Kanda ya Ziwa, Kaskazini, Kusini na karibu na Bahari ya Hindi kuchukua tahadhali hiyo.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa kuanzia kesho Jumatatu Desemba 17, 2018 hadi Desemba 20, 2018 baadhi ya mikoa itaathiriwa na mafuriko jambo ambalo litafanya baadhi ya shughuli za kijamii kusimama.

“Hii inamaanisha kuwa mafuriko yatatokea katika maeneo mengi na kuathiri jamii nzima, kuvurugika kwa usafiri na barabara kubwa kutopitika, hatari kwa maisha kutokana na maji kujaa au yanayopita kwa kasi,” inaeleza.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad