KITENGO cha Biashara cha Mahakama Kuu, kimemwamuru mfanyabiashara Yusuf Manji na wenzake wanne kuilipa Benki ya Biashara ya Taifa (NBC) Sh. bilioni 33 kutokana na mikopo na madeni mbalimbali.
Katika kesi Namba 54 ya 2018 iliyoamliwa na Jaji Judge Butamo Philip, Manji na walalamikiwa Farm Equip (Tanzania) Company Limited, Tanperch Limited, Quality Group Limited na Kaniz Manji wanatakiwa kulipa jumla ya Sh. 15,982,193,605.23 ya madeni na huduma za uingizaji bidhaa hadi kufikia Februari 28, 2018.
Kwa mujibu wa rekodi za mahakama, katika mchakato huu, mkopaji mkuu alikuwa ni Farm Equip (Tanzania) Company Limited, wakati wadaiwa wenghine walikuwa ni wadhamini.
Katika kesi ya biashara Namba 56 ya 2018 iliyoamliwa pia na jaji huyo, mahakama ilimwamuru Manji na walalamikiwa wengine kuilipa benki hiyo Dola za Marekani 5,468,274.23 kama ziada ya madeni na riba. Mbali na Manji, walalamikiwa wengine katika kesi hii walikuwa Tanperch Limited, akiwa mkopaji mkuu, Quality Group Limited na Kaniz Manji kama wadhamini.
Kulikuwa na kesi nyingine ya biashara Namba 55 ya 2018 iliyomliwa na Jaji Barke Sahel ikihusu malipo ya Sh. 5,359,418,687.31.
Walalamikiwa katika kesi hii walikuwa Quality Corporation Limited akiwa mkopaji mkuu, wakati Quality Group Limited, Tenperch Limited, Yusuf Manji na Kaniz Manji walikuwa wadhamini wa Sh. 5,359,418,687.31 zilizotokana na mikopo hadi kufikia Februari 28, 2018.
Manji Yamkuta Mengine Atakiwa Kulipa Bilioni 33 Benki
0
December 11, 2018
Tags