Viongozi wa dunia na wageni mashuhuri wanawasili nchini Marekani kutoa heshima zao wakati wa mazishi ya rais wa zamani wa Marekani George HW Bush.
Mwili wa Bush ambao umekuwa kwenye bunge la Marekani, utahamishwa kwenda kanisa kuu la National Cathedral huko Washington baadaye leo Jumatano kwa mazishi.
Bush senior, ambaye alihudumu kama rais wa 41 wa Marekani kati ya mwaka 1989 na 1993 alifariki Ijumaa akiwa na miaka 94.
Atazikwa nyumbani kwao huko Texas kando na kaburi la mke wake Barbara.
Kipi kitafanyika kwenye mazishi?
Mazishi hayo yataanza huko Washington DC ,mwesndo wa saa tano asubuhi saa za Marekani.
Rais Donald Trump na mtangulizi wake Barack Obama, Bill Clinton na Jimmy Carter watahudhuria misa hiyo.
Mwanaufalme wa Wales, Chansela wa Ujerumani Angela, Merkel na mfalme wa Jordan Abdullah II ni kati ya viongozi wa dunia ambao watatoa heshima zao.
Viongozi wa zamani wakiwemo John Major, ambaye alihudumu kama waziri mkuu wa Uingereza wakati wa muhula wa Bush pia atahudhuria.
Mbwa wa Bush agusa wengi kwa kutoa heshima za mwisho
Leo Jumatano imetangazwa kuwa siku ya taifa ya kuomboleza na ofisi nyingi za serikali na soko la hisa la Marekani litafungwa.
Baada ya mazishi mwili wa Bush utasafirishwa kwenda Taxas ambao utakaa kwa umma hadi Alhamisi asubuhi.
Mazishi ya George HW Bush: Viongozi Wawasili Kutoa Heshima Zao
0
December 05, 2018
Tags