Mbunge Lema Aomba Spika Tulia Ashughulikiwe na Bunge, Baada ya Kuimba Wimbo Mwanza Nyegezi

Video inayosambaa mtandaoni ikimuonyesha Naibu Spika wa Bunge, Dr. Tulia Ackson Mwansasu akiwa na Wabunge wanzake wakiimba wimbo ‘Mwanza’ wa muimbaji Rayvanny ambao umefungiwa na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), imezua gumzo mtandaoni.


Wabunge hao walikuwa nchini Burundi kwenye michuano ya wabunge na baada ya kuibuka na ushindi wakaanza kushangilia kwa style ya kuimba wimbo huo ambao upo kifungoni.

Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amefunguka kwa kudai kwamba, Mhe Spika Tulia anatakiwa kuhojiwa na kamati ya maadili ya Bunge kuhusiana na tukio hilo.

“Nina muomba Mh Spika Ndugai aitishe kamati ya maadili ya Bunge juu ya kitendo cha Naibu Spika Mh Tulia kuimba na kucheza wimbo uliopigwa marufuku na Basata unaoitwa Nyege,Nyege ,Nyegezi /Mwanza akiwa Nchini Burundi.Mimi na Mke wangu tume huzunika sana,”

Video hiyo ipo kwenye mtandao wa Instagram wa meneja wa Diamond, Babu Tale.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad