Mbwa wa Bush Awaguza Wqombolezaji Wengi Msibani

Mbwa was Bush Awaguza Wqombolezaji Wengi Msibani
Mbwa aliyekuwa amepewa kazi ya kuwa msaidizi wa Rais wa 41 wa Marekani George HW Bush amepigwa picha akionekana kuomboleza karibu na jeneza la kiongozi huyo.



Bush, aaliingia madarakani mwaka 1989 hadi 1993 alifariki dunia Ijumaa iliyopita usiku akiwa na miaka 94.




Sully, mbwa wa jamii ya golden labrador, alisafiri pamoja na mwili wa marehemu kwenye ndege kutoka Texas kwenda Washington DC siku ya Jumatatu.



Jeneza lenye mwili wake lilisafirishwa kwa ndege kutoka Texas kwenda DC kwa ndege ya Air Force One – ambayo kwa muda ilipewa jina Special Air Mission 41, kwa heshima ya rais huyo. Mwili huo ulirejeshwa Texas Jumatano.

Watu katika mitandao ya kijamii wamekuwa wakimshukuru Sully kwa huduma zake, na kwa kawaida kuzungumzia uaminifu wa mbwa kwa wamiliki wao. Watu katika mitandao ya kijamii wamekuwa wakimshukuru Sully kwa huduma zake, na kwa kawaida kuzungumzia uaminifu wa mbwa kwa wamiliki wao.


Sully amepewa jina la rubani wa ndege za abiria Chesley “Sully” Sullenberger, ambaye alifanikiwa kuielekeza ndege ya kubeba abiria kutua kwa dharura kwenye Mto Hudson mwaka 2009, na kuwaokoa abiria wote 155 na wahudumu waliokuwa kwenye ndege hiyo.

Mbwa huyo mwenye miaka miwili alikabidhiwa jukumu la kuwa mbwa msaidizi wa Bush aliyekuwa akitumia kiti cha magurudumu mapema mwaka huu.


Sully ni mbwa aliyepokea mafunzo sana, na anaweza kutekeleza maagizo mengi, ikiwemo kufungua milango na kuchukua vitu vinavyohitajika na mmiliki wake, mfano simu inapoita. Sasa atahudumu kama mbwa msaidizi kwa wanajeshi waliojeruhiwa vitani.

Sully ana ukurasa wake kwenye Instagram, na hapa anaoneshwa akimsaidia Bw Bush kupiga kura wakati wa uchaguzi wa katikati ya muhula mwezi jana.

Rais Bush amekuwa akipokea matibabu ya ugonjwa wa Parkinson na alilazwa hospitalini akiwa na tatizo la maambukizi kwenye damu mwezi Aprili. Alifariki akiwa na miaka 94 mjini Houston, Texas.

Atazikwa kwenye maktaba ya rais Texas, karibu na mkewe, Barbara Bush, aliyefariki dunia miezi saba iliyopita.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad