Meya Apinga Mti Unaowaka Moto Kukatwa

Meya apinga mti unaowaka moto kukatwa
Meya wa Manispaa ya Moshi Raymond Mboya amepinga kitando cha ukataji wa mti ambao ulikuwa unawaka moto bila kuzima nakusema kuwa bora ungeachwa utumike kama kivutio.

Meya huyo amesema hayo wakati akifanyiwa mahojiano na Chombo kimoja cha Habari na kusema kuwa hakubaliani na ukataji wa miti ovyo kwani mti mwingine unakatwa ukiwa na miaka zaidi ya mia na wanatoa sababu nyepesi.

" Kilichotokea kwa Mti kuwaka moto kwa siku tatu lakini moto unawaka hauunguzi majani na hatutaki kujiuliza ni moto wa aina gani na huu moto sio wakawaida lazima tuufanyie utafiti na Watu watataka kuja kuuona huu mti ni wa dizaini gani sio kuchukua maamuzi ya kuuangusha kwasababu huu mti unavyowaka utasababisha ajali'' alisema Mboya

Hata hivyo Meya Mboya aliendelea kusema Serikali haiamini ushirikina sasa wao walisema ungefanyika utafiti ili kujua kama ungeleta madhara au la, yeye anasema huo ni uharibifu wa mazingira kwa sababu ule mti una miaka mingi unazaidi ya miaka mia labda na wanasema ulikuwa una nyuki wengi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad