Mfungwa mmoja katika jimbo la Tennessee nchini Marekani atauawa kwa kiti cha umeme baada ya kudai kuwa sindano ya sumu itasababisha ateseke.
David Earl Miller, ambaye amekuwa kwenye hukumu ya kifo kwa miaka 36 ni kati ya wafungwa wanaoongezeka wanaojaribu kukwepa sindano ya sumu kufuatia visa kadhaa vya kufeli.
Mfungwa mwingine huko Tennessee Edmund Zagorski, aliuawa kwa njia ya umeme mwezi uliopita.
Kuuliwa kwa kutumia sindano ya sumu ndiyo njia kuu ya kuwaua wafungwa katika jimbo hilo.
Hata hivyo wafungwa katika jimbo hilo ambao walitenda uhalifu kabla ya mwaka 1999 wataruhusiwa kuchagua kuuliwa kwa njia ya umeme.
Mahakamani, Miller na Zagorski walitaja kisa cha kuuuliwa Billy Ray Irick cha mwezi Agosti ambaye alibadilika rangi kuwa Zambarau na kuchukua dakika 20 kufa.
Mfungwa mkongwe zaidi wa Nigeria aomba msamaha
Kuuliwa kwa Zagorski ilikuwa mara ya pili kiti cha umeme kimetumiwa katika jimbo hilo tangu mwaka 1960.
Miller alikutwa na hatia ya kumuua mwanamke aliyekuwa na matatizo ya akili mwenye miaka 23 mwaka 1981.
Ni kwa nini sindano ya sumu ina utata?
Miller, 61, na Zagorski, 63, walidai kuwa sindano hiyo ya sumu inayotumiwa na jimbo la Tennesee itasababisha kifo kirefu na chenye uchungu.
Hii ni baada mauaji kadhaa yaliyofanyika kwa kutumia mchanganyiko wa dawa ambapo wafungwa wameonekana wakiteseka.
Mwezi Septemba daktari mmoja aliiambia mahakama huko Tennessee kuwa Irick alihisi uchungu sawa na mateso wakati akiuawa.
Hata hivyo wale wanaounga mkono kutumika kwa sindano ya sumu wanasema haisababishi uchungu.
Miller pia ni mmoja wa wafungwa wanne waliohukumiwa kifo ambao wamepeleka kesi mahakamani wakitaka jimbo la Tennesee kutumia risasi badala ya sindano au umeme.
Katika jimbo jirani la Alabama, zaidi ya wafungwa 50 wamechagua kuuawa kwa kutumia gesi ya nitrogen badala la sindano ya sumu baada ya kuruhusiwa kuchagua mapema mwaka huu.
Ni majimbo yapi yanatumia kiti cha umeme?
Kutumika kwa umeme sio tena njia kuu ya kuwaua wafungwa katika jimbo lolote nchini Marekani.
Mfungwa ambaye alitumia ndugu yake pacha kutoroka jela Peru
Mahakama huko Georgia na Nebraska zimesema kuwa kiti cha umeme ni kinyume cha katiba.
Hata hivyo Miller ameambiwa kuwa hawezi kudai kuwa kiti cha umeme ni kinyume na katiba kwa sababu yeye mwenyewe amekichagua.
Kunyongwa ilikuwa njia kuu ya kuwaua wafungwa nchini Marekani hadi miaka ya 1890. Kisha kiti cha umeme kikaanza kutumika kwa wingi.
Mwaka 1982 matumizi ya kwanza ya sindano ya sumu yalifanyika katika jimbo la Texas na kuchukua taratibu mahala pa kiti cha umeme.
Mfungwa Achagua Kuuawa kwa Kutumika Kiti cha Umeme Badala ya Sindano ya Sumu
0
December 06, 2018
Tags