Mtandao wa ‘Go Pageant’ umetaja warembo 15 kati ya 113 waliochaguliwa kuwania taji la Miss World mwaka 2018 kuwa ndio wana nguvu au ushawishi mkubwa na kuna uwezekano mshindi akatoka katika Top 15 hiyo iliyotajwa na mtandao huo.
Miss Tanzania 2018 QueenElizabeth Makune katika list hiyo anashika nafasi ya nne ikiwa nafasi ya kwanza inashikiliwa na Shrinkhala kutokea Nepal, ya pili inashikwa na Dayana kutokea Pueto Rico na nafasi ya tatu inashikiliwa na Natalia kutokea Russia.