Mizengo Pinda Aibuka na Kuzungumza Maumivu ya Wapinzani

Mizengo Pinda Aibuka na Kuzungumza Maumivu ya Wapinzani
Waziri Mkuu mstaafu, Mizengo Pinda ameweka wazi jinsi alivyokuwa akiumizwa na kauli za upinzani dhidi ya uongozi wake na kusema kuwa anaushangaa upinzani kulalamikia uongozi amabo waliulilia kwa muda mrefu.

Akifungua Baraza la Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), Mkoa wa Dodoma, Pinda amesema kuna kipindi wakati wa uongozi wake, wapinzani walikuwa wakiinyooshea kidole serikali yao kuwa ni dhaifu haina makali, hivyo walikuwa wanataka kiongozi mkali na mwenye uamuzi mgumu.

"Kauli hiyo na ilikuwa ikinikera kwa sababu ilitulenga viongozi wa wakati ule, lakini sasa nashangaa kuona wapinzani haohao wameanza kulalamika tena juu ya utendaji kazi wa Rais John Magufuli ambaye ndiye kiongozi wa aina waliyekuwa wakitamani kumpata", amesema Pinda.

Pinda amesema kuwa, Rais Magufuli ndiye kiongozi ambaye Watanzania walikuwa wanamhitaji kutokana na uthubutu alionao katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.

Ameongeza kuwa, "Wakati fulani kuna baadhi ya watu huwa wananiuliza, hivi mzee na wewe si ulikuwa unautaka urais, nawajibu tu aka huyuhuyu ndiye anayefaa, mimi ni miongoni mwa watu wanaomkubali sana Magufuli".

Pinda aliteuliwa kuwa Waziri Mkuu na Rais wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete baada ya Edward Lowassa kujiuzulu. Mwaka 2015, alikuwa miongoni mwa wanachama wa CCM waliojitokeza kugombea urais lakini jina lake liliondolewa katika hatua za awali.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad