Klabu ya Manchester United ambayo jana ilimfuta kazi Jose Mourinho leo imemtangaza mchezaji wake wa zamani Ole Gunnar Solskjaer, kuwa kocha wa muda hadi mwisho wa msimu wa 2018/19.
Solskjaer ambaye aliichezea Man United mwaka 1996 hadi 2007, atasaidiwa na Mike Phelan, Michael Carrick na Kieran McKenna.
Baada ya uteuzi wake, wakongwe mbalimbali wa soka wametoa mitazamo yao juu ya uteuzi wa mwanasoka huyo wa zamani ambaye ni raia wa Norway mwenye miaka 45.
Mwandishi wa habari za michezo wa Teregraph, Paul Hayward amesema kitendo cha klabu kumrejesha kocha Mike Phelan ni hatua nzuri na kitasaidia kurejesha morali kwa timu hiyo.