Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania Hamza S. Johari leo Disemba 27, 2018 amezungumza na Waandishi wa Habari kuhusu Kampuni ya Fastjet kuzuiwa kuingiza ndege hapa nchini pamoja na tuhuma kibao walizozitoa wakidai AirTanzania inapendelewa.
1.FastJet hawakuwa na ndege hata moja hivyo kama mamlaka ya TCAA hatuna budi kuwazuia, wanamadeni ya 6 billion japo wamelipa kidogo, lakini sheria inawataka walipe yote, hivyo kama wao wanahitaji kufanya biashara wafuate masharti na walipe madeni.
2.Tulipata taarifa kupitia vyombo vya habari kwamba tarehe 22 Disemba 2018 wangeleta hizo ndege zao, lakini mamlaka haikuwa na taarifa hizo na wao utaratibu wa kuingiza ndege nchini wanaujua.
3.Ilipofika Tarehe 24 Disemba 2018 saa 6 mchana ndo wakatuma email ya maombi ya kuleta ndege hizo zenye usajili wa Afrika Kusin.
4.Ikumbukwe kwamba, tarehe 25 ilikuwa ni sikukuu na tarehe 26 ilikuwa ni Boxing Day hivyo sote hatukuwa ofisini. Wanaposema et tumewazuia kuzileta ni waongo.
5.Katika notisi ya siku 28 tuliyowapa, tuliwataka Fastjet walete andiko la kudhibitisha uwezo wa kufedha ili kuona kama wanajiweza na pia walete Meneja Mwajibikaji mwenye utaalamu na mambo ya ndege. Fastjet hawakuletea hivyo vitu
6.Badala yake Tar 24.12.2018 ndo sasa wakaleta maombi na barua ya mkurugenzi mtendaji wa Fastjet Lawrence Masha wakitujulisha kuwa Lawarence Masha amejiteua mwenyewe kuwa accountable manager.
7.Fastjet waache mzaha. FastJet itakufa kwasababu zao wenyewe maana wanamatatizo mengi, TCAA tunasimamia sheria ili kulinda usalama wa abiria, kulinda maslahi ya watoa huduma (supplies). Habari zote zilizoelezwa si za kweli ni upotishaji mtupu.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania AKANUSHA Tuhuma za Fastjet Kuzuiwa Kuingiza Ndege Nchini
0
December 27, 2018
Tags