Taarifa hiyo ya kuahirishwa mkutano wa 20 wa marais wa jumuiya hiyo uliokuwa ufanyike Desemba 27, 2018 imetolewa na mkuu wa mawasiliano kwa umma wa EAC, Richard Owora bila kufafanua sababu za kuahirishwa mkutano huo.
Mkutano wa awali ambao ulikua ufanyike Novemba 30 uliahirishwa dakika za mwisho wakati marais watatu wakiongozwa na Mwenyekiti wao Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta na Rais wa Tanzania, John Magufuli walipokutana.
"Mwenyekiti (Rais Yoweri Museveni) anaendelea na mashauriano na marais wenzake juu ya hatua zaidi," imesema taarifa hiyo.
Mkutano wa Novemba 30 haukufanikiwa baada ya nchi ya Burundi kugoma kutuma ujumbe kutokana na mgogoro wa kisiasa kati yake na jirani yake Rwanda.
Mkutano wa 20 wa Marais wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Waahirishwa Tena
0
December 22, 2018
Tags