RC Anna Mghwira amechukua uamuzi unaoelezwa kuwa umekidhi maazimio ya mkutano mkuu wa wanahisa wa benki hiyo ya ushirika uliofanyika Septemba 11, mwaka huu
Baada ya kuvunjwa kwa bodi hiyo Mkuu wa Mkoa aliitangaza kamati ya mpito itakayosimamia uendeshwaji wa benki hiyo kwa kipindi cha miezi mitatu tangu sasa
Mkutano mkuu wa wanahisa uliamua kuihamisha benki hiyo kutoka mfumo wa ushirika na kuirejesha katika mfumo wa kawaida wa uendeshaji