Rais Dkt. John Magufuli ameshangazwa na ufukwe wa Coco (Coco Beach) ulioko pembezoni mwa Bahari ya Hindi jijini Dar es salaam kutokuwa na choo wakati eneo hilo zinakusanywa fedha kila siku.
Akizungumza leo Disemba 20, 2018 kabla ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa daraja la Selander jijini humo, Rais magufuli amedai magari yanayoegeshwa kando ya fukwe hiyo hulipiwa shilingi 2,000.
“Coco Beach panatia aibu. Ifike wakati tuzizungumzie aibu zetu pale hakuna hata choo, ndio nasikia wanajenga sasa, bora Mkuu wa Mkoa umesema mtaanza kupaboresha pale Coco Beach, umeniwahi na una bahati, panatia aibu watu wanakwenda pale lakini hakuna hata choo?”, amesema Rais Magufuli.
Rais ameongeza kuwa, “Wanakusanya mapato kila siku hatujui hizo hela zinakwenda wapi na wanashindwa hata kujenga mabanda yaliyoboreshwa".
Hata hivyo, amesema Jiji la Dar es Salaam limebadilika na kuwa na sifa ya kuwa jiji la kibiashara, kwamba anafurahi kuhamia Dodoma akiacha Dar es Salaam ikiwa katika hali hiyo.
Si coco Beach pekee, public toilets ziongexwe dar and Tanzania kwa ujumla
ReplyDelete