Mkuu wa Wilaya wa Dodoma Ataka Wabunge wa Upinzani Wajiuzulu

Mkuu wa Wilaya ataka wabunge wa upinzani wajiuzulu
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Vijana CHADEMA,(BAVICHA) ambaye sasa ni Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Patrobasi Katambi amewataka wabunge wa vyama vya upinzani nchini kuachia ngazi nafasi zao za ubunge, kwa kile alichokidai kuwa wamekuwa wakilalamikia juu ya uhuru wa Tume ya Taifa ya

Uchaguzi ambayo iliwapitisha kuwa washindi wa kwenye majimbo yao.

Katambi ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na www.eatv.tv iliyotaka kujua juu ya ukimya wake baada ya kuhamia CCM na kupewa nafasi ya uongozi serikalini, tofauti na alivyokuwa katika chama chake cha zamani cha CHADEMA.

"Sijawahi kuvisema vibaya ila nilikuwa nasema ukweli, kwa sababu walikuwa wanalalamikia kuhusu tume huru ya uchaguzi ili waweze kuwathibitishia watanzania wajiuzulu ubunge wao, na nafasi nyingine za kisiasa ili tujue walipatikana kwa tume haramu, madai yao kwa sasa ni kupinga maendeleo lakini sisi tulifanya kisayansi," amesema Katambi.

"Kuhusu Nape Nnauye na Bashe, wao walikuwa wanazungumzia kuhusu maendeleo ya nchi lakini wabunge wa upinzani wengine ni vibaraka kwa sababu walikuwa wanapinga maendeleo," ameongeza.

Hivi karibuni kupitia www.eatv.tv Katambi alisema "kuwa ukimkuta mtu mtaani anafanya uhalifu, na ukikuta watu wanazungumza kwamba tunawadhalilisha kwa kweli hawana nia njema na jamii yetu, ndiyo maana sisi tunachofanya tunawaonesha ili waweze kurudi kwenye jamii kama watu safi,".

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad