Mnyika Ampongeza Rais Magufuli....Ataka Busara Itumike Kuwalipa Fidia Waliokumbwa na Bomoabomoa

Mnyika Ampongeza Rais Magufuli....Ataka Busara Itumike Kuwalipa Fidia Waliokumbwa na Bomoabomoa
Mbunge wa Jimbo la Kibamba kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo, (CHADEMA), John Mnyika amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli kwa kuweza kuamua kujenga barabara ya njia nane.

Amesema kuwa Watanzania wamemuombea asiwe na kiburi, huku akisema Wananchi wana malalamiko juu ya Bomoabomoa ambapo amemuomba kutanguliza utu, wa Mwl. Nyerere mbele.

Aidha, Mnyika ameongeza kuwa maendeleo ni ya vitu lakini maendeleo zaidi ni ya watu huku akimtaka atafakari kuwalipia fidia Wananchi waliopisha ujenzi huu.

“Kuna hili suala la bomoabomoa tunaomba ubinadamu utumike kwa kuwalipa fidia wananchi ili kuondoa malalamiko yaliyopo,” amesema.

Mbali na suala hilo la bomoabomoa,  Mnyika pia amemuomba Rais Magufuli kuondoa vikwazo vinavyoikabili demokrasia nchini.

”Demokrasia na Maendeleo ni mapacha, tunakuomba Rais unapofanya kazi za Miradi ya Maendeleo vilevile ukatumia fursa hii kuzungumzia kuondoa vikwazo vinavyoikabili Demokrasia ya Nchi ambayo tunaamini vitasaidia Nchi kusonga mbele,”amesema Mnyika

Pia ameongeza kuwa kuna mambo matano yanatoka kwa mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ambayo anawaomba Watanzania na Rais kwa ujumla kuweza kuyatafakari kwa muda huu tunapoelekea mwaka 2019.

Hata hivyo, Mnyika amesema kuwa akisikia Wafanyakazi wa Umma wanalilia kikokotoo, wengine wamepandishwa madaraja hawajapandishwa mishahara, Wafanyabiashara wanalia Mtaani, na kumuomba akipata nafasi ya kuzungumza pamoja na uzinduzi utatoa matumaini ya Taifa kwa 2019 na 2020″

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad