Moyo Wasahaulika Ndani ya ndege
0
December 14, 2018
Inaripotiwa kuwa ndege hiyo ilikuwa imepaa angani kwa karibu saa tatu
Ndege ya abiria ya Marekani iliyokuwa ikisafiri kutoka mji wa Seattle kuenda Dallas ililazimika kukatiza safari baada ya moyo wa binadamu kusahaulika ndani yake.
Shirika la ndege la Southwest linasema kuwa kiungo hicho kilisafirishwa Seattle kutoka California, ambako ilitarajiwa kutolewa mishipa ambayo ingetumiwa baadaye kwa utaratibu wa tiba ya upandikizaji.
Lakini kisanduku ambacho kilikuwa kimehifadhi moyo huo kilisahaulika ndani ya ndege hiyo na hilo lilifahamika baada ya ndege kuanza safari kuelekea Dallas.
Kisa hicho kilitokea siku ya Jumapili lakini kiliangaziwa katika vyombo vya habari siku ya Alhamisi.
Abiria waliyokuwa ndani ya ndege hiyo wanasemakana kushutuka sana wakata rubani alipowaambia kuhusiana na mzigo huo na kwamba hana budi kugeuza mkondo na kurejea walikotoka.
Baadhi yao walitumia simu zao kujifahamisha kuhusu muda ambao moyo unaweza kuhifadhiwa kabla ya itumike kwa upasuaji- kwa mujiu wa wataalamu, moyo wa binadamu huchukuwa kati ya saa nne na sita kuharibika.
Ndege hiyo iliripotiwa kupaa angani kwa karibu saa tatu.
Daktrai mmoja aliyekuwa miongoni mwa wasafiri na ambaye hakuwa na uhusiano wowote wa kusafirisha kiungo hicho aliiambia gazeti la Seattle Times, kwamba tukio hilo ni ''utepetevu wa hali ya juu''.
Baada ya ndege hiyo kutua salama mjini Seattle, moyo huo ulipelekwa katika kituo cha afya cha kuhifadhiwa.
Gazeti hilo liliongeza kuwa kiungo hicho kilipokelewa na kuhifadhiwa katika muda uliyostahili
Tags