Msaada Wangu kwa Mke wa mtu Miaka 2 iliyopita Unahatarisha Ndoa Yangu Mpya

Nitawapa kisa chenyewe kwa ufupi sana, maana sitaki kuwachosha.

Ni hivi, kuna jamaa tumeishi naye jirani tangu akiwa hajaoa mpk alipo oa tukaendelea kuwa majirani kwa miaka 4. Baadaye wakawa wamepata senti kidogo wakajenga kibanda chao sehemu, kama km 4 kutoka makazi ya mwanzo.

Huko wakaendelea kuishi lkn bila ya kupata mtoto. Mwaka wa saba wa ndoa yao, 2015, mkewe akaja kwangu kunishirikisha matatizo yao, na kisha kuniomba nitembee naye ili apate mtoto. Nilikataa.

Akaendelea kuniomba mwaka mzima. Kwakuwa kidume nilikuwa sijaoa na hata mchumba sina wakati huo, nikaona ngoja nipige mzigo. Nikala mzigo mara kadhaa kisha akadaka mimba.

Furaha ndani ya nyumba yao iliongezeaka sana, na wakamshukuru sana Mungu. Mwanaume akanunua ng'ombe dume na kumtolea Mungu sadaka ya shukurani kanisani. Mke akatunza siri kweli kweli nami nikawa busy na mambo yangu.

2017 mwezi wa pili mtoto akazaliwa, wa kiume. Vigele vigele, shangwe na nderemo vikapigwa, na mapenzi yakaongezeka baina yao.

Kinacholeta shida hivi sasa ni kwamba "chapa" yangu imejitokeza. Yaani, mtoto yuko kopi kopi na mimi. Na jamaa ananijua vizuri maana tumeishi naye. Mtoto amefichua siri kwa rangi, sura na kimo. Ugomvi mkubwa umezuka.

Wakati ugomvi huo ukiibuka huko, mm ndiyo kwanza ndoa yangu ina miezi 9 tu. Na mume wa mtu amepanga kuja kumwaga mboga kwa mke wangu, hii ni kwa mujibu wa mkewe. Amenipigia simu kunitahadharisha.

Waungwana nifanyeje kuepukana na kadhia hii?
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad