Msako Mkali wa Silaha Kuanza Zanzibar....Wanaozimiliki Kinyume na Utaratibu Wapewa Siku 5 Kuzisalimisha

Jeshi  la Polisi Zanzibar, limetoa siku tano kuanzia jana kwa watu wanaomiliki silaha kinyume na utaratibu wazisalimishe katika vituo vya polisi visiwani humu.   Limesema baada ya kipindi hicho, litafanya operesheni ya kuwatafuta wamiliki hao na kuwachukulia hatua.   Kauli hiyo ilitolewa na Kamishna wa Polisi Zanzibar, Mohamed Haji Hassan na kusema kwa upande wa Zanzibar, silaha zilizoruhusiwa kutumiwa ni shotgun na gobore huku bastola zikiwa zimeruhusiwa kutumika Tanzania Bara.   Kamishna huyo aliwataka wanaomiliki bastola ambazo hufanya mipango kwa Tanzania Bara na kuingia nazo Zanzibar kutokana na sababu mbalimbali, kuzisalimisha kwenye vituo vya polisi.   “Kwa wanaomiliki bastola ambazo wamefanya mipango yao huko Tanzania Bara wanatakiwa kuzisalimisha na hawatakiwi kubaki nazo nyumbani kwani kwa kufanya hivyo ni uvunjifu wa sheria,” alionya Kamishna huyo.   Alisema Jeshi la Polisi limepata taarifa ya kuwepo kwa watu wanaomiliki silaha hizo kutojasajiliwa, hivyo aliwataka wale ambao silaha zao hazijasajiliwa wazisalimishe Makao Makuu ya Polisi Zanzibar katika kipindi hicho.   Alisema endapo kuna mtu anayetaka kuingia Zanzibar na bastola lazima akaisalimishe polisi na ataruhusiwa kuondoka nayo atakapoamua kurejea Tanzania Bara, kinyume na hivyo atakuwa anatenda kosa.   Kamishna Hassan aliongeza kuwa kwa mujibu wa sheria namba 2 ya mwaka 2015 ya Zanzibar kifungu cha 31 (1) kinachohusu udhibiti wa silaha za moto na milipuko, Kamishna wa Polisi ana mamlaka ya kufanya usajili wa silaha ndogo kwa matumizi binafsi.   Alisema silaha zilizoainishwa katika sheria kwa ajili ya matumizi au uwindaji wanyama waharibifu wa mazao shambani na si kwa matumizi mengine.   “Lengo la kuzuia silaha hizo ni kuimarisha ulinzi kwa raia na mali zao ambapo wapo baadhi ya watu ambao hutumia silaha hizo vibaya na kusababisha uvunjifu wa amani
Jeshi  la Polisi Zanzibar, limetoa siku tano kuanzia jana kwa watu wanaomiliki silaha kinyume na utaratibu wazisalimishe katika vituo vya polisi visiwani humu.

Limesema baada ya kipindi hicho, litafanya operesheni ya kuwatafuta wamiliki hao na kuwachukulia hatua.

Kauli hiyo ilitolewa na Kamishna wa Polisi Zanzibar, Mohamed Haji Hassan na kusema kwa upande wa Zanzibar, silaha zilizoruhusiwa kutumiwa ni shotgun na gobore huku bastola zikiwa zimeruhusiwa kutumika Tanzania Bara.

Kamishna huyo aliwataka wanaomiliki bastola ambazo hufanya mipango kwa Tanzania Bara na kuingia nazo Zanzibar kutokana na sababu mbalimbali, kuzisalimisha kwenye vituo vya polisi.

“Kwa wanaomiliki bastola ambazo wamefanya mipango yao huko Tanzania Bara wanatakiwa kuzisalimisha na hawatakiwi kubaki nazo nyumbani kwani kwa kufanya hivyo ni uvunjifu wa sheria,” alionya Kamishna huyo.

Alisema Jeshi la Polisi limepata taarifa ya kuwepo kwa watu wanaomiliki silaha hizo kutojasajiliwa, hivyo aliwataka wale ambao silaha zao hazijasajiliwa wazisalimishe Makao Makuu ya Polisi Zanzibar katika kipindi hicho.

Alisema endapo kuna mtu anayetaka kuingia Zanzibar na bastola lazima akaisalimishe polisi na ataruhusiwa kuondoka nayo atakapoamua kurejea Tanzania Bara, kinyume na hivyo atakuwa anatenda kosa.

Kamishna Hassan aliongeza kuwa kwa mujibu wa sheria namba 2 ya mwaka 2015 ya Zanzibar kifungu cha 31 (1) kinachohusu udhibiti wa silaha za moto na milipuko, Kamishna wa Polisi ana mamlaka ya kufanya usajili wa silaha ndogo kwa matumizi binafsi.

Alisema silaha zilizoainishwa katika sheria kwa ajili ya matumizi au uwindaji wanyama waharibifu wa mazao shambani na si kwa matumizi mengine.

“Lengo la kuzuia silaha hizo ni kuimarisha ulinzi kwa raia na mali zao ambapo wapo baadhi ya watu ambao hutumia silaha hizo vibaya na kusababisha uvunjifu wa amani

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad