Msanii Auawa Kwa Kisu na Mpenzi wake
0
December 14, 2018
Msanii wa vichekesho nchini Kenya ambaye ni maarufu kwenye igizo la 'Vioja Mahakamani', Jamal Nasor, ameuawa baada ya kuchomwa kisu na mpenzi wake aliyetambulika kwa jina la Grace Kananu.
Tukio hilo ambalo limetokea Disemba 12 katika eneo la Athi River, kaunti ya Machakos nchini humo, limeelezwa kuwa wawili hao walikuwa wakigombana, ndipo Grace alipoamua kumshambulia kwa kumchoma kisu na kujemruhi na kupelekea kifo chake.
Baada ya kufanya tukio hilo, mwanamke huyo alikimbia na kumuacha Jamal peke yake hadi alipokuja kuokotwa na wasamaria wema ambao walimpeleka hospitali ya Shalom mjini Machakos.
Polisi tayari wamemkata mshukiwa wa mauaji hayo na anatarajiwa kupandishwa kizimbani, kujibu mashtaka yanayomkabili.
Jamal ambaye pia alikuwa akiigiza kama Jaji kwenye igizo la 'vioja mahakamani' na kwenye vichekesho maarufu vya familia vinavyojulikana kama 'junior', mchekeshaji huyo alikuwa akiigiza kama 'Baba Junior'. Jamal Nasor amezikwa mjini Mombasa.
Tags