Mtibwa yashindwa rasmi safari, yawaachia Simba


Klabu ya soka ya Mtibwa Sugar imeshindwa kusonga mbele katika michuano ya shirikisho barani Afrika baada ya kukubali kichapo kutoka kwa KCCA ya Uganda kwenye ardhi ya nyumbani hii leo.

Mchezo huo uliopigwa katika uwanja wa Chamazi umeshuhudia Mtibwa ikikubali kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa timu hiyo ya jiji la Kampala. Mabao ya KCCA yamefungwa na Muzamiru Mutyaba katika dakika ya 28 na Allan Okello katika dakika ya 88 huku bao pekee la Mtibwa likifungwa na Salum Kihimbwa katika dakika ya 51.

Mtibwa imeondolewa michuano hiyo kwa uwiano (Aggregate) ya 1-4 kufuatia kupoteza mchezo wa awali kwa mabao 3-0 jijini Kampala wikiendi iliyopita.

Simba na Mtibwa ndiyo wawakilishi pekee wa Tanzania katika michuano ya vilabu barani Afrika msimu huu, ambapo sasa hatma imebakia kwa Simba inayoshiriki Klabu Bingwa barani Afrika katika mchezo wake wa kesho Jumapili dhidi ya Nkana Red Devils.

Katika mchezo wa kwanza, Simba ilipoteza kwa mabao 2-1 nchini Zambia, inahitaji bao moja pekee la ushindi kuweza kuwavusha hatua inayofuata ya makundi ya michuano hiyo.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad