Rais wa Uganda Yoweri Museveni amekutana na mlimbwende wa nchi hiyo ambaye hivi majuzi ameshinda taji la mlimbwende bora wa Afrika.
Quiin Abenakyo alitawazwa kuwa Miss Uganda mwezi Agosti na kushiriki shindano kubwa la ulimbwende duniani la Miss World nchini Uchina mwezi huu ambapo aliingia kwenye tano bora na kutawazwa taji la Miss Africa.
Rais Museveni alimsifia mlimbwende huyo na waandaji wa shindano la Miss Uganda na kuahidi kuwapa ushirikiano. Lakini hata hivyo 'alimsuta' mrembo huyo kwa kuvaa "nywele za Kihindi".
"Abenakyo ni mrefu haswaa, binti mrembo kutoka Musoga. Tatizo langu pekee ni kuwa alikuwa amevaa nywela za Kihindi. Nimemsihi kubaki na nywele zake za asili. Lazima tuuoneshe uzuri wa Kiafrika katika uhalisia wake," ameandika Museveni kupitia ukurasa wake rasmi wa Twitter.
Ruka ujumbe wa Twitter wa @KagutaMuseveni
View image on Twitter
View image on Twitter
Museveni 'Amsuta' Mlimbwende Aliyeshinda Taking la Miss Bora Afrika kisa kuvaa wigi
1
December 20, 2018
Tags
Namuunga mkono Rais Musaveni 100%, dada zetu ni wazuri sana lakini mambo mengine kama nywele za bandia, mikorogo kuwa eti weupe wanaharibu "Beauty nature" uzuri asilia wa Kiafrika lakini utasikia ma "westerner" wanalaumu eti "Haki za ubinadamu" mbona wao hawajipaki rangi nyeusi au kuvaa wig za kiafrica??
ReplyDelete