Mwalimu Ahukumiwa Miaka Mitatu Jela kwa Kosa la Kupokea Mshahara Mara Mbili

Mwalimu Ahukumiwa Miaka Mitatu Jela kwa Kosa la Kupokea Mshahara Mara Mbili
Mahakama ya Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu, imemhukumu kifungo cha miaka mitatu jela pamoja na kurejesha Sh milioni 10.3, Mwalimu Josiah Mkome baada ya kukutwa na hatia katika kesi ya uhujumu uchumi iliyokuwa inamkabili.

Mwalimu Mkome alikuwa akifundisha Shule ya Sekondari Kandawe wilayani Magu, mkoani Mwanza alishtakiwa kwa kosa la kupokea mishahara miwili kutoka katika Wilaya ya Magu na Maswa kinyume cha sheria.

Mwendesha mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) wa Mahakama ya Wilaya ya Maswa, amedai mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo Fredrick Lukuna, mshtakiwa alipokea mishahara hiyo miwili tangu Februari mwaka 2012 hadi Mei mwaka 2015.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad