Mwana FA amtaja Mwandishi Bora wa Mashairi Afrika Mashariki

Mwana FA amtaja Mwandishi Bora wa Mashairi Afrika Mashariki
Msanii mkongwe wa Hip Hop Bongo, Mwana FA amefunguka kuwa yeye ndiye mwandishi bora zaidi wa mashairi hapa Bongo, Afrika Mashariki na ukanda mzima wa nchi za maziwa mkuu.

Mwana FA amelazimika kuweka wazi hilo leo kwenye Planet bongo ya East Africa Radio alipokuwa amesimama kwenye 'Heshima ya Bongo fleva' ambayo pia huwa inaruka 'LIVE' kupitia East Africa Television kuanzia saa 8:00 hadi saa 9:00 kila siku ya Ijumaa.

''Mimi ni mwandishi bora japo ni mtazamo wangu binafsi na mwingine anaruhusiwa kuwa na mtazamo wake lakini mashairi yangu huwa yanaeleza uandishi wangu huwa ni 'deep' kiasi gani'', amesema FA.

Mwana FA ambaye yupo kwenye 'game' kwa miaka 17 sasa amesema kama mtu ana wasiwasi na uandishi wake basi atakuwa si msikilizaji mzuri wa mashairi, hivyo akasikilize tena ataelewa kwanini anasema yeye ni bora.

Amemaliza kwa kusema anajipanga kuachia ngoma nyingine baada ya kuwa kimya kwa mwaka mzima tangu alipoachia ngoma yake ya mwisho 'Hata sielewi' ambayo alimshirikisha Maua Sama.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad