Binti huyo Humeyra Öz alivamiwa katika eneo la kuegesha baiskeli kwenye chuo cha ubunifu huko Rotterdam muda mfupi baada ya kumaliza masomo yake Jumanne mchana.
Mwanaume wa miaka 31 tayari amekamatwa.
Rafiki wa kike wa binti huyo wanasema ni kijana ambaye alisha achana nae muda mrefu sana na alisha lalamika kutishiwa na kijana huyo.
Polisi wamethibitisha kuwa alimjua mtuhumiwa lakini hawakutoa taarifa za ziada.
Tukio hili limetokeaje?
Kituo hicho cha ubunifu kina wanafunzi 300, na baadhi yao walikuwa katika eneo la baiskeli muda ambao tukio limetokea na waliona kilichotokea.
Binti huyo aliyeuawa pamoja na mtuhumiwa wote walitambulika kuwa wanatoka katika jamii ya waholanzi wenye asili ya Kituruki, na afisa balozi Aytac Yilmaz alitembelea shule hiyosiku ya jumatano.
Wanafunzi wenzie walikuwa na wakati mgumu kuamini tukio hilo, wakati wazazi walikua na hofu ya usalama wa watoto wao.
"Alikuwa na upendo, mzuri sana na ana akili," rafiki yake wa shule ameviambia vyombo vya habari uholanzi
"Bado tuna hofu sana. Mauaji haya yametokeaje?"
Mwenyekiti wa chuo hicho maalumu kwa ubunifu anasema ilikua ngumu kuzungumzia vitisho alivyopewa marehemu kwasababu ilikuwa ni mikononi mwa polisi, lakini amesisitiza kuwa usalama katika shule hiyo haukuwa na tatizo.